Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyoshi: Nimeanza kupaka Mkorogo toka Darasa la Sita

NYOSHI EL SAADAT THE BOGOSS ARUMBAYA Mwanamuziki wa kikongo, Nyoshi El Saadat

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa kikongo, Nyoshi El Saadat (Rais wa vijana) anasema alianza kuchubua ngozi ya uso wake kwa mkorogo tangu akiwa darasa la sita, hivyo anawashangaa wanaomuona wa ajabu huku akidai kujichubua kwake ni kujipamba kama wanamuziki wengi wa Congo wafanyavyo.

“Sioni ajabu kupaka mkorogo, nimeanza tangu nikiwa darasa la sita hadi leo ni miaka mingi, pia napaka kwa kuwa ni mwanamuziki ninayejua kujipamba nashangaa wanaonishangaa, we huoni yangu ngozi imetulia na kuwa na mvuto kwa sababu natumia vipodozi vya gharama ambavyo mtu mwingine hawezi kumudu gharama hizo.

“Gharama zake ni kubwa, naweza kutumia Mkorogo wa laki tatu hadi tano kwa kuwa nachanganya vitu vingi na naweza kukosa vvote lakini mkorogo lazima uukute kwenye kabati langu la vipodozi,” anasema Nyoshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live