Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyieeee! Eti Dida kapata mchumba tena, kufunga ndoa ya tano!

DIDA KUOLEWA Nyieeee! Eti Dida kapata mchumba tena, kufunga ndoa ya tano!

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama unadhani Dida yupo singo unakosea kwani kwa kinywa chake amekiri kuwa yupo na mwenzake ambaye tayari wapo kwenye mchakato wa kuelekea kwenye ndoa.

Dida amekiri hilo leo Agosti Mosi, 2023 kwenye Kipindi cha Mashamsham alipohojiwa na watangazaji wenzake wambeya kina Juma Lokole.

"Ndio tuna kama miezi sita hivi tangu tuingie rasmi kwenye mahusiano. Tulianza muda kutongozana, tulikuwa tunachati hivi lakini baadaye tukaingia rasmi," alisema Dida bila kumtaja jina la mwanaume wake huyo.

Ikiwama mambo yataenda vizuri kama Dida alivyosema basi hii huwenda itakuwa ni ndoa ya tano kwa mtangazaji huyo. Ameolewa na kuachika na mabwana tofauti. Wa mwisho kumuoa alikuwa ni Meya wa jiji la Dar, Omary Kumbilamoto.

Hizi hapa ndoa nyingine za Dida zilizowahi kuvunjika;

DIDA NA MCHOPS

Awali, kabisa akiwa chini ya umri wa miaka 20, Dida aliolewa kwa ndoa ya kifahari na mfanyabishara maarufu jijini Dar aliyeitwa Mohammed Mchopanga almaarufu Mchops.

Wawili hao walipendana na kapo yao ikawa maarufu kiasi cha Dida kupewa jina la Dida wa Mchops ambalo hadi leo kuna watu wanamuita hivyo.

Katika ndoa yao, Dida na Mchops walijaaliwa kupata mtoto wa kike mkubwa tu kwa sasa aitwaye Samira kabla ya kuachana kwa kile kilichodaiwa ni kushindwana.

DIDA NA G

Baada ya hapo, mwaka 2011, Dida alifunga ndoa ya pili na mfanyabiashara Gervas Mbwiga almaarufu G na ndipo likazaliwa lile jina la Dida wa G.

Ndoa hiyo ilidumu kwa mwaka mmoja tu kabla ya kuvunjika mwisho mwa mwaka 2012.

DIDA NA EZDEN

Kutoka kwa G, Dida akatua moyo wake kwa Jumanne Ezden ambaye wakati huo alikuwa Mtangazaji wa Tevisheni ya TV1.

Katika kuachana kwao, kila mmoja alitoa sababu zake huku Dida akidai kupokea vipigo kutoka kwa jamaa huyo ambaye kwa upande wake alidai kujifunza mengi kutoka kwa mwanamama huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live