Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyie! Whozu amjibu Tunda kwa Wema+VIDEO

Whozu Na Wema Nyie! Whozu amjibu Tunda kwa Wema+VIDEO

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama itakuwa ni kweli, basi huwenda muigizaji Wema Sepetu atakuwa naye ameamua kutafuta faraja yua kimahusiano kwa kuingia kwenye penzi la bwa’ mdogo Whozu.

Whozu alikuwa kwenye mahusiano na Tunda na kufanikiwa kupata mtoto mmoja kabla ya kuibuka drama mpya mjini zikimuonesha mrembo huyo yupo kwenye penzi jipya na msanii wa Singeli, Meja Kunta.

Klipu inayotrend huko mjini YouTube kwa siku ya leo, inamuonesha Wema akiwa na ameegemea mguu wa Whozu huku kijana wa watu akiwa amelembua macho kuonesha yupo kwenye ulimwengu wa mbali sana kimahaba.

“Siamini kama kweli Wema anaweza kutoka na huyu mtoto.” Mmoja wa watu walichangia kwenye kipande hicho cha video.

Wapo wengine waliompongeza Wema kwa kumpata mwenza na kumtakia kila lakheri ikiwezekana amzalie mtoto.

View this post on Instagram

A post shared by Tanzania Web (@tanzaniaweb)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live