Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyashinski aongoza Bongo Apple Music Top 100 Songs

Rapper Nyashinski Nyashinski.

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tovuti ya Kworb.net hutoa ripoti za chati za muziki kutoka kwenye majukwaa tofauti ya kusikilizisha muziki.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, wimbo wa muimbaji na rapa wa Kenya, Nyashinski – Perfect Design, ndiyo wimbo namba moja Apple Music Tanzania. Perfect Design ni wimbo wa nne kutoka kwa Nyashinski mwaka huu; baada ya kuziachia Beautiful, Good To Me na Moment Of Bliss ambazo ziliifuata EP ya Nyashiski ‘Therapy’.

Video ya Perfect Design ilikuwa Premiered Oktoba 25; na kwa siku zilizopita, video hiyo imetazamwa zaidi ya mara 927k huku ikiwa kwenye nafasi ya 22 kati ya video 100 za muziki zinazovuma YouTube Tanzania.

2. Darassa – I Don’t Care

Darassa ni miongoni mwa wanamuziki wa Bongo fleva waliofanya ‘wandaz’ mwaka huu, nyimbo kama ‘Nobody’ feat. Bien, Dead Zone, na ‘Mind Your Business’ zimeumiliki mwaka kwa ukubwa ule ule ambao Darassa amekuwa akiupata anaporudi kwenye masikio ya mashabiki wa ladha ya muziki wake.

Wimbo ambao unampa Darassa muda mwingi wa kusikilizwa wakati huu ni ‘I Don’t Care’. Wimbo huo ulioachiwa wiki tatu zilizopita, upo kwenye nafasi ya pili kati ya nyimbo 100 zinazosikilizwa zaidi Apple Music Tanzania.

3. Asake – Lonely At The Top

Nafasi ya tatu kwenye orodha ya nyimbo100 zinazosikilizwa sana Apple Music Tanzania ni ‘Lonely At The Top’ wa Asake. Wimbo huo umeweka rekodi ya wimbo uliomiliki namba 1 kwa muda mrefu zaidi kwenye TurnTable Top 100, ambao ndio mfumo pekee wa jumla wa chati nchini Nigeria unaochanganya redio, TV na majukwaa ya ku-stream.

4. Marioo – Shisha Feat. Mr. Nice

Wimbo mwingine wa Bongo fleva unaoendelea kujikusanyia maelfu ya wasikilizaji Novemba hii, ni Shisha wa Marioo akiwa amemshirikisha mfalme wa Takeu Style, Mr. Nice. Ukiwa na wiki mbili tangu kuachiwa, Shisha umeshikilia nafasi ya 4 kwenye nyimbo 100 za Apple Music Tanzania huku ikionyesha ishara zote za kuendelea kufanya vizuri kwenye chati hiyo.

5. Alikiba & Tommy Flavour – Huku

Alikiba na kijana wake Tommy Flavour wameendelea kuwa kwenye masikio ya wasikilizaji wa Bongo Fleva, wimbo wao ‘Huku’ ni miongoni mwa nyimbo za Bongofleva zenye mashabiki wengi mwisho wa mwaka huu; ipo kwenye orodha yetu ya nyimbo zinazotabiriwa kugombea wasikilizaji na nyimbo zitakazoachiwa mwanzoni mwa mwaka 2024.

Nafasi kumi za juu za chati hiyo zimepambwa na Top 5 tuliyokuandikia hapo juu, huku Crayon & Ayra Starr kwenye ‘Ngozi’ wakiwa nafasi ya sita. Nafasi ya saba imeshikiliwa na Kamo Mphela, Tyler ICU & Khalil Harrison – Dalie (feat. Baby S.O.N).

Wimbo mpya wa Harmonize, ‘Sijalewa’ upo nafasi ya nane huku jina la Diamond Platnumz likionekana kwenye nafasi ya tisa na wimbo wake ‘Shu! (feat. Chley)”. Burna Boy na wimbo wake wa ‘City Boys’ anaifunga 10 bora ya nyimbo 100 zinazosikilizwa zaidi Apple Music Tanzania juzi Novemba 1, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live