Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nusura niigize filamu za ngono - Majid Michael

Majid Michel 63e64b9037d46.jpeg Majid Michael

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa filamu Bongo, Majid Michael amedai kuwa wakati wa kujitafuta ilifika wakati akataka kushawishika kuigiza filamu za ngono ili tu apate umaarufu.

Majid Michael ameongeza kuwa kwa sasa anafanya kazi hiyo huku akilinda heshima yake.

"Watu wengi wapo tayari kufanya chochote kwa ajili ya kuwa maarufu, wasichojua ni kwamba umaarufu ni kama gereza.

"Nilivyoanza kuigiza kama kijana mtanashati nilifanya kila nilichoambiwa, niliigiza hadi filamu zilizonitaka nijidhalilishe. Sikufikiria kesho yangu.. Ila niliposhawishiwa kuigiza filamu za ngono, Mungu akanigusa, nikakataa mara moja,"

"Sasa nimejifunza kukataa kuigiza mambo yatakayoniharibia brand yangu. Nataka sanaa yangu isije ikafanya watoto wangu na wajukuu wangu wasinitazame usoni. Nataka niwe bora na mfano wa kuigwa," amesema Majid Michael.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live