Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nusu ya wanawake katika muziki wanakabiliwa na ubaguzi - ripoti

Nusu Ya Wanawake Katika Muziki Wanakabiliwa Na Ubaguzi   Ripoti Nusu ya wanawake katika muziki wanakabiliwa na ubaguzi - ripoti

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Nusu ya wanawake katika tasnia ya muziki wanakabiliwa na ubaguzi kulingana na ripoti iliyotolewa.

Chuki dhidi ya wanawake, ubaguzi wa kijinsia na unyanyasaji bado ni matatizo ya kila siku kwa wanamuziki wa kike nchini Uingereza, ripoti mpya ya kusikitisha imegundua.

Inasema kwamba thuluthi moja ya wanawake katika tasnia ya muziki wamenyanyaswa kingono kazini, huku wengi wakiripoti kuwa ni kikwazo kwa taaluma zao.

Wanawake pia wana uwezekano wa kukabiliwa na ubaguzi mara nane zaidi kuliko wanaume.

Matokeo hayo yanatoka kwa Sensa ya kwanza kabisa ya Wanamuziki wa Uingereza, iliyofanywa na Muungano wa Wanamuziki.

Ilichunguza zaidi ya wataalamu wa tasnia ya muziki 6,000, kati yao 2,526 walitambuliwa kama wanawake.

Ripoti ilisema wanawake wanalipwa kiwango cha chini kuliko wanaume, na mara nyingi wanapata kazi kwa muda mfupi, licha ya kufundishwa na kuelimishwa kwa kiwango cha juu.

Zaidi ya robo ya wanamuziki wa kike (27%) walisema hawakupata mapato ya kutosha kutokana na muziki kuendeleza taaluma, ikilinganishwa na 20% ya wanaume.

Kwa wastani, wanawake hupata 10% chini ya wenzao wa kiume, na wastani wa mapato ya kila mwaka ya £ 19,850 ikilinganishwa na £ 21,750 kwa wanaume.

Chanzo: Bbc