Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nuh Mziwanda ashindwa kuachia EP kisa usimamizi

Nuh Mziwanda Ep Nuh Mziwanda

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Nuh Mziwanda, leo amefunguka na kusema anawashangaa wasanii wanaotoka kwenye lebo (usimamizi), wakati huko kuna afadhali kuliko kujisimamia mwenyewe.

Nuh Mziwanda ameenda mbali zaidi na kusema kuwa ameshindwa hata kuachia EP (Extended Playlist) yake kutokana na kukosa usimamizi.

“Mimi nilitangaza kuachia EP ila mpaka sasa ishakua BP kwangu maana kila mtu ana mtu wake, Nawaonea huruma sana mnaotoka kwenye Usimamizi,” ameandika Nuh Mziwanda.

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii mbalimbali kuvunja mkataba na lebo zilizokuwa zinawasimamia kwa sababu mbalimbali ambazo nyingi hazijawekwa wazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live