Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Noel: Mimi sio chawa Diamond

Noel Na Diamond Noel: Mimi sio chawa Diamond

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo maarufu Bongo Noel Ndale, amefunguka kwamba, kuna watu wamezusha kwamba haonekani mara kwa mara na wasanii kama zamani hivyo kuwajibu kwamba yeye sio chawa wa msanii.

Noel amesema, yeye kazi yake ni ubunifu wa mavazi na sio kitu kingine sasa baadhi ya watu huwa wanatamani kwamba kila wakati wamuone ameambatana na wasanii.

“Wabongo wanapenda hayo mambo ya uchawa. Mimi sio chawa. Huwezi kuniona na msanii lakini nipo, naendelea kufanya kazi na wasanii pale ninapokuwepo. Nafanya kazi na Diamond, kama kuna kazi amefanya na sijashariki basi ujue nilikuwa sipo,” alisema Noel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live