Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Njiwa peleka salamu nilirekodi 1980" - Patricia

Bi Hl "Njiwa peleka salamu nilirekodi 1980" - Patricia

Fri, 18 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

HitMaker wa wimbo wa 'Njiwa peleka salamu' Bi Patricia Hillary amefunguka kwamba wimbo huo aliurekodi mwaka 1980 lakini uzuri wa wimbo huo ukichezwa mahali ni kama umetoka siku za hivi karibuni.

Submitted by Shaluwa Anta on Ijumaa , 18th Jun , 2021 Bi Patricia Hillary kwenye studio ya East Africa Radio

Akizungumzia historia ya wimbo huo kwenye Heshima ya Planet Bongo ya East Africa Radio Hillary Patricia amesema 

"Wasanii wa sasa waangalie tungo zao wanazotunga ziwe za muda mrefu, kama mimi njiwa peleka salamu nimeirekodi mwaka 1980 lakini mpaka sasa bado ina utamu wake"

"Nilimtumia njiwa kwa sababu ni ndege nzuri lakini wakati nauandika wimbo huo nilikuwa nimemshika mkononi na naongea nae kabisa, nilikuwa najisikia vizuri sana na watu walipenda huenda ndio alileta uzuri wa wimbo huo". ameeleza Bi Patricia Hillary   

Chanzo: eatv.tv