Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Njia 3 kukabili ongezeko la gharama za maisha

Cover Image (1) (1) Njia 3 kukabili ongezeko la gharama za maisha

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hata bila takwimu za kukusanywa na kishikwambi, kila kona nchini kuna malalamiko na manung’uniko juu ya kupanda mno kwa gharama za maisha.

Hivi sasa kama unasikiliza watu, wengi wao wanaishi maisha yasiyo na matumaini na wana machungu mioyoni mwao.

Hata hivyo, kama wewe ni mmojawao, basi usitie shaka, jinsi hali ilivyo ngumu huwa ni fursa ya kujinasua nayo, hapa chini nakupa njia 3 unazoweza kuzitumia kukabili makali ya ongezeko la gharama za maisha;

Nunua unachoweza kudhibiti kukitumia; ili uendelee na maisha yako ya kawaida kama awali, unatakiwa kujua ni kitu gani unamiliki na ni rahisi kiasi gani kukuwezesha kukitumia mara kwa mara.

Kuanzia kwenye aina ya chakula unachokula, unatakiwa kujua kama unaweza kumudu kila siku.

Fanya manunuzi yako kwa wingi; kama unaweza kufanya manunuzi yako mara moja kwa mwezi, hiyo ni nzuri kwako kwa sababu unakuwa upande wa kulia wa kupanga bajeti, aina hii ya ununuzi itakuruhusu kupanga cha kufanya baadaye.

Kuwa na side hustle; kama umeajiriwa ni lazima uweze kutafuta upande wako ili usitegemee chanzo kimoja tu cha pesa kukulisha wewe na familia yako, jaribu sana kupata moja utaweza kuona jinsi itakavyosaidia kulisha familia yako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live