Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Nipo tayari kuolewa na mwanaume yeyote - Isha Mashauzi

Isha Mashauzi 2 Isha Mashauzi

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki nguli wa taarabu na Mjasiriamali katika sekta ya Upishi, Isha Mashauzi amesema kufuatia kuolewa ndoa mbili na kuishia kuachika huku ndoa yake ya mwisho ikidumu kwa muda wa miezi kadhaa tu.

Isha aliolewa 2009 akaachika 2010, amesema kwa sasa hana tena muda wa kuchagua na kutoa vigezo kwa mwanaume wa kuwa naye kwenye mahusiano kwasababu umri wa kuweka vigezo umepita.

Amesema kwa sasa yupo tayari kuwa kwenye mahusiano na mwanaume yeyote, awe amemzidi umri au awe chini ya umri wake yote kheri, yeye anachoangalia ni upendo wa kweli.

Isha amejinadi kuwa yeye bado ni Mlimbwende, bado anatishia kwa uzuri hata asipopakaa mekap na kikubwa anachojivunia kwenye mwili wake ni ukubwa wa matiti yake aliyojaaliwa na mwenyezi Mungu.

Isha amesema kila akiamka asubuhi cha kwanza lazima akague maziwa yake maana ya walimwengu ni mengi sasa hivi unaweza ukaamka ukakuta matiti yako yapo kwenye chungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live