Msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohammed 'Shilole' amefunguka kuwa licha ya kuwa na mwili mkubwa lakini ana mwili wa kitoto jambo ambalo linamfanya mumewe, Rommy 3D kutokaa mbali naye.
Shilole ambaye huwa ahishiwi vituko amesema mwili wake ni wa kitoto hivyo muda wote unamfanya mumewe huyo kujikuta akimbusu mashavuni kila wakati wawapo nyumbani.
"Nina mwili mkubwa lakini Mungu kanijalia baby face, sura yangu imekaa kitoto sana na inavutia kwakweli, tukiwa nyumbani kazi ya mume wangu ni kunibusu mashavu muda wote kwa sababu yanavutia, namshukuru Mungu kwa huu upekee alionipa," amesema Shilole.