Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Nina mpango siku yoyote kuzivunja tuzo za KTMA nilizoshinda’ – AT

Thu, 4 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Msanii wa muziki wa Miduara kutoka Zanzibar Ally Ramadhani aka ‘AT’ amesema ana mpango wa kuzivunja tuzo zote alizowahi kushinda kupitia Category mbalimbali kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) sababu amesema kuwa haoni faida ya tuzo hizo kwa sasa.

AT amezungumza kwenye XXL ya Clouds FM kwa kusema>> ‘Yaani nina mpango siku yoyote zile tuzo za KTMA nazivunja,sitakaa na tuzo hata moja sizitaki sababu kila nikizona na matukio ambayo yapo najisikia vibaya sana sababu naamini ningekua nimepiga hatua’

Sentensi zingine alizosema AT >> ‘Sababu ni watu ambao wanasema mtu yoyote akija tutamsaidia lakini mimi nimekwanda pale pamoja na kuwa nilikua na ahadi walishindwa kunisaidia,nikaona wananidharau haina haja ya kubaki na  makopo, siku nitakayovunja nitaweka Instagram, Hawawezi kunishtaki zile tuzo ni za kwangu’ -AT

#TwoFiveFive

Msanii wa Muziki wa mduara AT, kutoka visiwani Zanzibar amesema kuwa atazivunja zawadi ya Tuzo alizopewa na Tanzania Music Award sababu haoni faida yake.

— Clouds Media (@CloudsMediaLive) January 3, 2018

Unajua kama AT na Dayna Nyange hawakumchagua Rais Magufuli? Wameyazungumza haya kwenye uongozi wake.

Chanzo: millardayo.com