Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Nimepata bahati, sikulazimishwa" - Hamisa Mobetto

59061 Mamahamisapic "Nimepata bahati, sikulazimishwa" - Hamisa Mobetto

Fri, 8 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na mrembo Hamisa Mobetto amesema, amepata bahati ya watu kumfuatilia na watoto wa kike kumuangalia kama kioo chao licha ya kuzaa watoto wawili na wanaume tofauti nje ya ndoa.

Akieleza wakati anapewa ubalozi wa Afya ya Uzazi ya Sitetereki, amesema kupitia yeye wasichana wanadhani kuzaa ni rahisi kwa kuonekana kama amepata mtoto, mwili umerudi na maisha yanaendelea lakini ni ngumu kuliko wanavyofikiria.

"Nimepata bahati ya kutizamwa, kufuatiliwa na kuwa na mashabiki wengi, watoto wengi wa kike wananiangalia mimi na kudhani kwamba ni rahisi kuzaa mtoto, mwili umerudi na maisha yanaendelea na kuona mambo ambayo tunawaonyesha lakini ni vigumu sana kuliko wanavyofikiria" ameeleza Hamisa Mobetto.

Aidha akizungumzia kuhusu kupata watoto wawili nje ya ndoa na wanaume wawili tofauti amesema "Mtoto ni mipango ya Mungu lakini pia sikulazimishwa, nilikuwa nipo tayari na kwa ratiba zangu nilishajua kwamba nitazaa mtoto kwa muda fulani kisha nitarudi kwenye kazi zangu ndiyo maana watu wengine wanaona ni rahisi kufanya".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live