Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimemtoa Hemed Phd lakini hajawahi kusema - Natasha Mamvi

Hemed Phd Sax Nimemtoa Hemed Phd lakini hajawahi kusema - Natasha Mamvi

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe kwenye tasnia ya bongo movie @natashamamvi wengi wakimjua kama mama yake Monalisa leo amefunguka na kusema kuwa yeye ndio aliyemtoa kisanaa kwenye uigizaji mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri kwenye sanaa Hemedy Phd @hemedyphd

Natasha amesema kuwa yeye ndio aliona kipaji cha Hemedy na kusema kuwa anaweza kuigiza na kuwa msanii mzuri, lakini Hemedy Phd hakuwahi kusema popote kama alitolewa na Natasha

Natasha alisema," Nina miaka 25 kwenye sanaa, nilitumia miezi sita kuonekana kwenye kamera kipindi hicho na kuna watu wengi nimewainua kwenye sanaa, mmoja wapo ambaye sijawahi kumsikia akisema sehemu ni Hemedy Phd, tulimpa sinema na tulienda mpaka kwa mama yake kumuomba ila sijamsikia popote akisema na mimi ndio mtu wa kwanza kumwambia Hemedy you are a good actor na nashukuru anaperform vizuri mpaka sasa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live