Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimempa Ibraah huu mwezi wa Oktoba pekee - Harmonize

Nimempa Ibraah Huu Mwezi Wa Oktoba Pekee   Harmonize.png Nimempa Ibraah huu mwezi wa Oktoba pekee - Harmonize

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa lebo ya muziki wa Konde Music Worldwide, Harmonize amesema kwamba amelazimika kupunguza kasi ya kuachia vibao katika mwezi huu wa Oktoba na kutoa fursa hiyo kwa msanii wake Ibaah.

Harmonize ambaye alikuwa anazungumza baada ya tamasha ililohudhuriwa pia na bosi wake Jembe alisisitiza kwamba Oktoba hatokwenda kuachia vibao vingine tena bali ameitoa nafasi hiyo kwa Ibraah ili pia kuunguruma baada ya kimya cha karibia mwaka mzima.

Hata hivyo, msanii huyo alisema kuwa hiyo haimaanishi amefulia bali anakuja kurudi kumalizana kabisa na washindani wake wa kimuziki kabla ya kuununja mwaka.

“Konde Gang tumepata changamoto tofauti tofauti ambazo zilimfanya Ibraah akachelewa kidogo kutoa miziki yake lakini amekuwa akirekodi sana. Kwa hiyo mimi najua anachoenda kukifanya kwenye muziki huu mwaka lakini na mimi pia nimempa huu mwezi mzima wa Oktoba angurume, atie magoma kabla mimi sijaenda kumalizana nao,” alisema.

Harmonize pia alisisitiza kwamba wao kama wasanii kutoka lebo ya Konde Music Worldwide watalazimika kuweka mipaka ili wasiwe wanafanyiwa mzaha katika kazi zao za muziki.

“Nadhani tunachoenda kukifanya sisi kama Konde Music Worldwide ni kuweka tu mipaka ijulikana kwamba sisi ndio hawa, wengine ni hawa na hawa, unajua muziki wetu unazidi kua kila siku, keki inakuwa kubwa na kila mtu ana nafasi ya kufanya anavyojisikia,” alisema.

Aliwaahidi mashabiki wake kwamba kinachoenda kufanyika mwisho wa huu mwaka ni bora hata asikisema na mashabiki wakisubiri tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live