Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimekuwa Zari The Boss Lady kabla sijawa na Diamond – Zari

3779 14449152 1807308329504796 7769537358189297664 N 1 TZW

Tue, 27 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amesema mara baada ya kuachana na muimbaji huyu ameamua kuendelea na biashara zake kwani carrier yake ilikuwepo kabla ya kuwa katika mahusiano na Diamond.



Mrembo huyo akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC amesema anaendelea na maisha yake ya kuandaa event pamoja ku-host na anatarajia kuja na realty show yake inayokwenda kwa jina la Life of Zari The Boss Lady.

“I do a lot of things, kwanza ujue even before nimemkuta Diamond, nimekuwa nafanya appearances, nimekuwa Zari The Boss Lady even before Diamond, so I continue nitakuwa nafanya appearances, nitakuwa nafanya show, so I continue do the same thing,” amesema Zari.

Katika hatua nyingine Zari amefunguka iwapo hiki kinachoendelea ni kiki au kina ukweli wowote, Zari amesema kinachoendelea ni ukweli mtupu na kabla ya kutangaza uamuzi wake wa kumuacha Diamond walikaa wiki tatu bila kuzungumza.

“Yaani tumeachana kabisa it’s done, tangu zile video zimetoka na ex wake (Wema Sepetu) nikawa nimempiga block at a time, tukawa hatujaongea three week after that ndio nikaposti, nimeamua nijiweke kando kabisa, I don’t need to be emotional, so I don’t real to speak more about this issue,” ameeleza.

Alipoulizwa iwapo Diamond ameshamuomba msamaha au yupo tayari kumsamehe, alijibu; “Ameshakuja kipindi fulani, kipindi amezaa na yule dada fulani (Hamisa Mobetto), so sasa hivi sidhani kama inawekezana tena.”.

Chanzo: bongo5.com