Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimejifunza mengi kwa Mkapa - Ditto

D02f79fc4bdb4c0e55a8713effef2f4c Nimejifunza mengi kwa Mkapa - Ditto

Wed, 29 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Lameck Ditto ‘Dogo Ditto’ amesema amejifunza mambo mengi hatayasahau kwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ditto alisema miongoni mwa mambo aliyojifunza ni maendeleo makubwa aliyoyafanya Rais Mkapa kwa taifa na msimamo wake lakini kingine ni kitabu alichokiacha kikielezea historia ya maisha yake kinachoitwa My Life, My Purpose.

Alisema kifo chake kimewagusa Watanzania kwa sababu ya kile alichokifanya kwenye sekta mbalimbali nchini.

“Kumpoteza ni pigo kubwa kwa taifa hili kwa sababu alikuwa mtu muhimu aliyetufanyia mambo mengi ya kitaifa, ametuachia kitabu cha maisha yake unajifunza vizuri ukisoma, tumshukuru kwa hilo kwani kile kitabu ni kioo,” alisema.

Ditto ni miongoni mwa wasanii walioibuliwa na rapa Afande Sele mwaka 2003 katika tamasha la kuibua vijana wadogo wenye vipaji lililoandaliwa na kituo cha Redio Ukweli kilichokuwa na makao yake Morogoro.

Aliwahi kuvuma na nyimbo kadhaa zikiwemo Moyo sukuma damu, Sioni haya, Wapo, Darubini Kali akishirikiana na Afande Sele uliowahi kukamata chati katika ukanda wa Afrika Mashariki na nyingine nyingi.

Pia ndio mtunzi wa nyimbo za Tuulinde Muungano na Tanzania zilizoimbwa kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali.

Chanzo: habarileo.co.tz