Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niliumia baba kutomzika mama yangu - Dimpoz

Ommy Dimpoz Nn.png Niliumia baba kutomzika mama yangu-Dimpoz

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa Bongo Omary Nyembo ‘Dimpoz’ amesema maisha aliyopitia na marehemu mama yake yalikuwa magumu lakini pia aliumia sana kitendo cha baba yake mzazi kushindwa kuhudhuria mazishi ya mama yake.

Dimpoz amefunguka hayo kupitia kipande cha video alichokiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo amefafanua mambo mbalimbali kuhusu uhusiano wake na baba yake.

“Niliumia sana kitendo cha yeye kutofika kabisa kwenye mazishi ya marehemu mama yangu. Hakutaka hata kuja kujua mimi nitaishije baada ya mama kufariki nikiwa primary,” alisema Dimpoz.

Dimpoz amesema, ameona baba yake akifanyiwa mahojiano na Cloudstv akidai wanabusti tamasha la Fiesta lakini kimsingi yeye hana mapenzi baba yake kwa sababu alimtelekeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live