Mlimbwende na Mjasiriamali aliyewahi kuwa mpenzi wa Aslay na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike, Tessy Chocolate amesema kwa sasa amejipata kimaisha kwani bidhaa zake za Momo Beauty zinafanya vizuri sokoni na amefanikiwa kuzisambaza mikoa yote ya Tanzania.
Akijibu swali la kwa nini hayupo karibu na Irene Uwoya kama walivyokuwa zamani, Tessy amesema baada ya kuvunjiwa Saloon yake na watu wasiojulikana alijikuta akiwa kwenye hali ya simanzi na maswali mengi ya kutaka kujua ni nani alifanya kitendo hicho lakini mpaka leo bado hajamtambua mbaya wake aliyeamua kumuharibia maisha.
Amesema baada ya tukio hilo alijikuta akijitenga na marafiki zake wote aliokuwa nao kipindi hicho na miongoni mwa watu aliowapungua Uwoya alikuwa miongoni mwao, Tessy amesema hana ugomvi na Uwoya na wala hawakugombana kisa mwanaume kama watu wanavyodhani ila ni wakati tu ulifika wa kupunguzana ili maisha mengine yaendelee na anayaona matunda ya maamuzi yake.
Kuhusu kurudiana na mzazi mwenzie Aslay, Tessy amesema hilo haliwezi kutokea kwani wakati wanaachana tayari walikuwa wamemalizana kwa kila kitu hivyo haitokuja kutokea wakarudiana na isitoshe ni miaka mitano sasa tangu waachane, hata hivyo licha ya kutengana na kila mtu kuwa na mahusiano yake mengine.
Tessy amekili kwamba Aslay ni baba bora kwa mtoto wake kwani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mwanae anaishi, anasoma na anakula vizuri, ndiyo maana hata yeye amekuwa mstari wa mbele kumsapoti baba mtoto wake huyo pindi anapoachia kazi zake za kimuziki.