Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilitegemea ningekuwa na TV kama Diamond na viwanda vikubwa – Juma Nature

8505 Juma Nature Diamond Bongo5 Pix TZW

Thu, 31 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii Juma Nature amesema albamu zake nyingi hasa ile ya Ugali ilifanya vizuri sokoni ila hajanufaika kama iliyotakiwa.



Nature katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm amesema kama si hivyo kwa sasa angekuwa miongoni mwa wasanii wenye mafanikio makubwa.

“Katika uuzaji ule wa nakala kwa kweli tulikuwa tunafunikwa funikwa tu, hatukupaswa kuwa hivi,” amesema.

“Nilitegemea pengine kwa kipindi kama hiki yaani mimi mwenyewe ningekuwa na TV zangu kama ulivyomuana Diamond alivyofanya, tena na viwanda vikubwa vyakwangu mwenyewe,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa hata vichache anavyomiliki kwa sasa na wasanii wengine wa zamani ni kwa vile waliamua kukomaa. Nature kwa sasa anatamba na ngoma mpya ‘Unayumba’ ambayo amemshirikisha Miss Makupa.

Loading...
Chanzo: bongo5.com