Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilishamwambia Wema atakuja kupata mtoto – Chuchu Hansy

Wed, 31 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Baada ya baadhi ya mashabiki kumtolea maneno yasiyofaa Wema Sepetu pindi alipoweka picha ya mtoto na Chuchu Hansy katika mtandao wa Instagram, muigizaji huyo amesema Wema hapaswi kuumizwa na hilo kwani utafika wakati wake atapata mtoto.



Chuchu Hans ameiambia E-Newz ya EATV kuwa Wema ni rafiki yake na mara kadhaa wao kama wanawake wamekuwa wakiongea na kumshauri na kumtia Moyo.

“Nilishamuambia wewe (Wema) utakuja kupata mtoto il sio pale unapohitaji wewe, ni pale ambapo Mungu amekuandikia muda wako ukifika, kwa hiyo hayo maneno wala asimuumie ni changamoto na kutokana na ustaa alionao,” amesema.

Mtoto wa Chuchu Hansi anaitwa ambaye amezaa na muigizaji mwenzake, Ray Kigosi.

Chanzo: bongo5.com