Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilipopata ujauzito sikuwa najua – Dayna Nyange

3687 24274462 883909168451916 8802991890736611328 N TZW

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Dayna Nyange amefungua tetesi za kuwa mjamzito.



Hitmaker huyo wa ngoma ‘Komela’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kwa sasa hana ujauzito ila anachokumbuka kwa sasa ni ujauzito wake wa kwanza ambao aliupata akiwa na umri wa chini ya miaka 18.

“Nilipopata ujauzito sikuwa najua, nilikuwanahisi ni Malaria nikaambiwa niende kupima pale hospital ile karatasi ya majibu nilipewa nikambiwa nipeleke nyumbani nilipofika nilimkabidhi dada yangu sikujua kama ni majibu kuwa ni ujauzito,” amesema Dayna.

Dayna ameongeza kuwa mtoto wake kwa sasa ana umri wa miaka 11 na anahitaji afike mbali kielimu asiwe kama yeye ambaye alishindwa kumaliza elimu ya sekondari.

Siku ya wapendanao (Valentine Day) February 14 mwaka huu aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram ambayo ilipelekea wengi kudhani Dayna ni mjamzito.

Chanzo: bongo5.com