Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Niliowaangusha mnisamehe" - Ray C

Ryc "Niliowaangusha mnisamehe" - Ray C

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Msanii wa kike na mkongwe kwenye BongoFleva Ray C amewaomba msamaha mashabiki zake ambao aliwaangusha kipindi cha nyuma kwa sababu yeye ni binaadam hajakamilika na anakosea.

Ray C ametoa ujumbe huo baada ya kifo cha rapa wa Marekani DMX ambapo chanzo cha kifo kifo chake ni kudaiwa kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya na mshtuko wa moyo.

"Naandika huku nalia sijui kwanini, nadhani ni hisia za ukweli tu niliwaangusha kipindi fulani mnisamehe maana mimi ni binadamu, waliolia na mimi ni wengi hilo nalijua na nawapenda sana ingawa wengine hatufahamiani ila nashukuru kwa kuendelea kunipenda na kuendelea kuwa pamoja nami kwa miaka yote" ameandika Ray C 

"Nawaheshimu kama mashabiki na kama binadamu wenzangu, upendo udumu ndani ya mioyo yetu hata siku mkiandika lala salama Ray C na kuniposti basi iwe kutoka moyoni" ameongeza

Ikumbukwe Ray C ni mmoja wa wasanii waliwahi kutumia madawa ya kulevya ila anamshukuru Mungu kwa kumtoa katika janga hilo ambalo linaharibu vijana wengi kukatisha ndoto zao na kusababisha kifo.

Chanzo: eatv.tv