Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilinyooshewa vidole kuwa nina Ukimwi - Mke wa Prof. Jay

Professor Jay, Mkewe Washerehekea Maisha Na Afya Prof. Jay na mkewe.

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa nguli wa hipo na mwanasiasa nchini, Profesa Jay aitwaye Grace Mgonjo amesema kuwa wakati mumewe akiwa mgonjwa, alisingiziwa kila aina ya jambo, hali iliyomfanya kujipa moyo na kumtumaini Mungu.

Grace Mgonjo amesema hayo mara baada ya mumewe kupona tena baada ya kukaa hospitali kwa siku 462 akiugulia maradhi ya figo yaliyokuwa yakimsumbua.

"Kipindi ambacho mume wangu anaumwa nilikuwa napitia wakati mgumu sana, lakini nilikuwa karibu na Mungu, ndugu walikuwa wakinifariji.

"Maneno ya watu nje yalikuwa mengi. Wakati mwingine unasikia amefariki wakati huo upo nyumbani au njiani unachanganyikiwa unafika hospitali unamkuta yupo sawa.

"Nilikuwa nanyooshewa vidole kuwa nina Ukimwi. Nilishawahi kusingiziwa kila kona kuwa nina Ukimwi. Ni kitu ambacho kimeshakaa nikasema ngoja nimuachie Mungu yeye ndiye anayejua," amesema Mke wa Profesa Jay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live