Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilimwambia mpenzi wangu atoe mimba-Country Wizzy

Country Wizzy Nilimwambia mpenzi wangu atoe mimba-Country Wizzy

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Country Wizzy ameweka wazi kuwa kwa mara ya kwanza alivyosikia kuwa mpenzi wake ni mjamzito hakuwa tayari kabisa na alichanganyikiwa.

Kwenye kipindi cha FreshWeekend cha Wasafi FM, Country aliulizwa vitu ambavyo vimetokea kwenye mahusiano yake ambavyo hawezi kuvisahau.

"Nilidata kwa sababu sikuwa tayari mimi kupata mtoto. Nilimwambia mama yake atoe lakini akakataa. Siku zilivyokuwa zinakwenda mimi kila mwezi nilikuwa nadata. Nilikuwa naogopa sana mtoto.

"Lakini hata hivyo nilikuja kufurahi sana alipojifungua na mimi nikawa baba daah nilifurahi sana," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live