Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilimuacha mume wangu sababu ni mwaminifu kupita kiasi

Kaka Celico (4).jpeg Kaka na Celico

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa zamani wa staa wa soka wa Brazil Ricardo Kaka, Caroline Celico amefichua siri ya kuachana kwao kuwa mumewe huyo wa zamani alikuwa mwaminifu kupitiliza ndio maana bibie aliomba talaka.

"Kaka hakuwahi kunisaliti, alinifanyia vizuri, alinipa familia nzuri, lakini sikuwa na furaha, kuna kitu kilikosekana. Tatizo lilikuwa ni moja tu, alikuwa ni mwanaume mkamilifu mno kwangu, umalaika wake ulinishinda nikaomba talaka" – Caroline.

Celico na Kaka walikuwa wapenzi tangu utotoni na walidumu kwenye ndoa kwa miaka 10 na kupata watoto wawili kabla ya kutalakiana mwaka 2015 ambapo Caroline ndiye aliyetaka talaka hiyo.

Wanaume mpo hapo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live