Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilimpa talaka mke wangu sababu alikuwa akiniroga - Mlilo

Mlilo Tre Nilimpa talaka mke wangu sababu alikuwa akiniroga - Mlilo

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara ya kwanza Msanii wa maigizo nchini Hussein Lugendo, maarufu kama 'Mlilo' amejibu tuhuma za kuachana na mkewe kisha kujituliza kwa Shamsa Ford ambaye pia ni kinara wa Filamu nchini.

Mlilo amesema yanayosemwa na aliyekuwa mkewe kwamba ameitelekeza familia siyo ya kweli, isipokuwa ukweli uliofanya wao waachani ni huu hapa.

Mlilo amesema awali walikuwa wanapendana vizuri yeye na mkewe lakini shida ilianzia pale alipogundua kuwa mkewe ni Mchawi na alikuwa anamroga kupitia waganga wa kienyeji, amesema aliambiwa na mganga kuwa mkewe alikuwa anamroga kwa namna tofauti, ndipo alipoanza kupunguza mapenzi taratibu kwa mkewe.

Siyo mambo ya uchawi tu, Mlilo amesema mkewe alikuwa kidomo-domo sana, walikuwa wakigombana kidogo mtaa wote wanajua na alikuwa ni mtu wa kuondoka kila mara wakigombana. Ameendelea kumdadavua na kumnyumbua mkewe ya kwamba alikuwa na wivu kwa Shamsa Ford ndiyo maana ndoa ilimshinda na sasa amekuwa mwanamke asiye na mume.

Amesema ni kweli alikuwa kwenye mahusiano na Shamsa Ford wakati ambao pia alikuwa kwenye ndoa (alikuwa anachiti), lakini hiyo ni kawaida na kila mwanaume aliyekamilika anajua kuchiti ni hali ya kawaida, lakini mkewe alishindwa kuvumilia akaambulia talaka tatu kwa mpigo.

Amempongeza Shamsa kuwa ni mwanamke mpambaji na mwenye pesa kiasi kwamba hata akipata shida Shamsa ni mwepesi wa kutoa msaada na kwa muda mrefu alikuwa anakatami apate Mwanamke wa kumsogeza mbele na siyo Mwanamke wa kukaa ndani kutwa nzima kama alivyokuwa akifanya mkewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live