Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nililala kitanda kimoja na mama yangu-Dimpoz

Dimpozzzzz Nililala kitanda kimoja na mama yangu-Dimpoz

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amefunguka kuwa, maisha aliyoyapitia zamani yalikuwa magumu kiasi cha kulala chumba na kitanda kimoja na mama yake.

Dimpoz amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiweka kipande cha video kuelezea jinsi alivyotelekezwa na baba yake mzazi ambaye sasa hivi anaonekana kuwa ana maisha ya hali ya chini kulinganisha na Ommy.

“Sina hata kumbukumbu kwamba hili daftari labda nilinunuliwa na baba yangu. Niliishi maisha magumu nikiwa peke yangu na mama yangu. Nililala chumba kimoja na mama,” alisema Dimpoz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live