Mwigizaji kunako tamthilia ya Juakali, Nyamaka maarufu kama Suzy amefunguka namna ilivyopitia misukosuko kwenye maisha yake hadi kufikia hatua aliyopo leo.
"Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye awali tulikuwa tunaishi vizuri, tulipendana sana na alikuwa akiniahidi mambo mazuri mazuri, baadae nilishika ujauzito wake na nikamwambia ukweli kwamba nina ujauzito wake, akaniambia sawa nitalea usiwe na wasiwasi"
"Aliendelea kunihudumia lakini mimba ilipofikisha miezi saba siku moja tukiwa tumekaa sehemu akaniambia 'bila shaka huyo atakuwa mtoto wa kiume' nikamuuliza kwanini unasema hivyo!! hata akiwa wa kike ni mtoto pia kikubwa tusubiri tuone Mungu anatuletea mtoto gani sisi tutampokea"
"Hakupendezwa na maneno yangu, ghafla akaacha kuwa karibu na mimi na hata pesa za matumizi akaacha kutoa, kuanzia hapo nilianza kuishi mwenyewe kwa tabu maana sikuwa na kitu maalumu cha kuniingizia pesa, hadi nafikisha miezi 9 nilikuwa choka mbaya kiuchumi, nilikuwa nimechakaa nimepauka kiasi kwamba hata ningetupwa kwenye kundi la mbwa wasingenila"
"Siku ya kujifungua nilimpigia simu kuwa najifungua, ajabu ni kwamba alinitumia elfu 50 tu wakati zilikuwa zinahitajika pesa nyingi na hapo alikuwa hajawahi kunitumia pesa tangu mimba ikiwa na miezi 7.
"Nilijifungua kwa tabu sana, baada ya kusikia nimejifungua akanipigia simu kuniuliza ni mtoto gani? nikamwambia wa kike, basi alikata simu kabisa akaacha hata kunijulia hali"
"Ukizingatia hakuwa na mtoto hata mmoja huyo ndiye alikuwa mtoto wake wa kwanza lakini alimkataa, nilipambana kwa shida hadi baadae nilipokutana na Lamata akanipa nafasi kwenye Juakali.
"Nikaanza kujilea mwenyewe hadi leo hii niko vizuri mtoto wangu anaishi vizuri, nimefungua Saloon na mtoto wangu atasoma shule nzuri nitamlea kwa uwezo wa Mungu," amesema Nyamaka.