Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee, amewashangaza wanamitandao baada ya kutangaza kuwa yupo singo kwa mara nyingine tena.
Mama huyo wa watoto watano ambaye mapema mwaka huu alifunga ndoa na Mswizi Dennis Schweizer aliyebandikwa jina Omosh, alielekea katika mtandao wake wa TikTok na kuchapisha ujumbe kuwa sasa yupo singo.
"Niko single tena" Akothee aliambatanisha ujumbe huo na emoji za kuvunika moyo na kulia.
Hata hivyo katika chapisho hilo, Akothee hakuibanisha aa kuelezea zaidi chanzo cha kutoa tangazo hli na kusimilia jinsi alivyojipata singo.
Siku ya alhamisi, hatua ya Akothee kujitokeza akiwa ameambatana na mpenzi wake wa zamani na meneja wake Nelly Oaks iliweza kuibua gumzo mitandaoni wengi wakionekana kutaka kufahamu ayupo wapi mume wake Omosh.
Hata hivyo, Mwimbaji huyo alikanusha kuwepo kwa mahusiano yoyote ya kimapenzi na kusema uwepo wa Oaks katika hafla hiyo ilikuwa ni kwa sababu alikuwa kama sehemu ya familia yake.
“Tunatoka mbali. Babu yake aliacha urithi katika jamii yangu. Unapomwona Nelly karibu nami, sijali unachotaka kufikiria.. Nelly asante kwa kuwa kila wakati kwa chapa ya Akothee na kwa kuwa kila wakati kwa watoto wangu. Anawatunza watoto wangu. Wanatoka pamoja, wanacheza densi. Wanangu wanampigia simu kila siku. Unapotuona, sisi ni familia," alisema.
Akothee ni mama wa watoto watano, wasichana watatu na wavulana wawili, ambao wote alipata na wapenzi wake wa zamani watatu.