Kumekuwa na Minong'ono ya chini chini kwamba eti @mbosso_ na @marioo_tz Huwa wanapandishiana nyimbo, yaani Mmoja Akitoa Leo basi mwingine anaachia kesho
Akijibu kuhusu hilo @mbosso_ amesema; "Ukifuatilia Kwa ukaribu utagundua kuwa nikitoa wimbo na yeye (Marioo) anatoa" lakini kwenye biashara ya Muziki ni ngumu kuamua tu kesho natoka wimbo."
#Mbosso ameendelea na kusema kuwa unapaswa kuwasilisha wimbo wiki mbili kabla hivyo akisikika msanii anazungumza kauli hiyo anashangaa sana.
Kuhusu ukaribu wao Mbosso ameweka wazi kuwa wawili hao ni washkaji kama siku zote Licha ya @marioo_tz kusema kuwa anaona kama Kuna tofauti Kati Yao (akiwa kwenye interview ya #TheSwitch).