Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nikitaka kazi naanza wiki ijayo – Mwana FA

1738 26340295 1278781565600807 5495642991487877120 N TZW

Mon, 22 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Mwana FA amefunguka changamoto alizowahi kupitia hadi kufikiria kuacha muziki na kwenda kuajiriwa.



Rapper huyo ameiambia Clouds Fm licha ya changamoto hiyo bado hakuajiriwa ila ni kitu ambacho hakihitaji ni muda wowote kukikamilisha.

“Mimi kuna kipindi nilikuwa na wakati mgumu kwenye muziki na nikafikiri muziki wenyewe nataka kuuacha nifanye shughuli zangu nyingine bahati nzuri mimi nina backup kabisa,” amesema Mwana FA.

“Ningeweza kutoa vyeti vyangu nikaendelea na shughuli nyingine fresh, nina backup na nina connection za kutosha mimi nikitaka kuanza kazi naanza wiki ijayo kama ninataka kwenda kazini saa mbili mpaka saa 11, yaani sio suala la kujiuliza,” amesisitiza.

Hata hivyo ameongeza kuwa anafahamu fika hata akienda kazini hamna popote anaweza akaenda duniani akakuta tambarare, hivyo kitu cha muhimu ni wasanii kufanya kwa moyo kile wanachokifanya bila kukata tamaa.

Chanzo: bongo5.com