Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nikikutana na Rais Magufuli nitamwambia afunge mitandao ya kijamii Tanzania – Steve Nyerere

8381 STEVE345 TZW

Mon, 28 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa filamu Steve Nyerere amedai anatamani kukutana na Rais Magufuli ili amshauri azime data, ili watu wasitumie mitandao ya kijamii kwa kufanya umbea na kuongea habari za uongo za kuchafuana.



Muigizaji huyo amedai Watanzania wanaacha kutumia fursa zinazotoka na mitandao ya kijamii na kubaki wakifanya majungu na umbea.

“Bado tunahitaji kuwa na mwenendo wa China, nitafurahi sana siku Magufuli akizima data, na nadhani kuna haja ya kumshauri Mheshimiwa Rais,” Steve Nyerere aliiambia kipindicha Enewz cha EATV. “Kwa sababu kama tunataka kujenga Tanzania ya viwanda, ni lazima siku moja tuzime data hata mwezi nadhani tutafikia malengo, tena andika kabisa Nyerere anatamani kuonana na Magufuli amnong’oneze kuhusu data, azime tu hata nwezi, ili watu wafanye kazi, amesema Steve Nyerere.

Aliongeza “asilimia 90 wanaishi kwenye mitandao na kubuni vitu ambavyo haviingizi taifa hata pato, nia ni kuliongezea taifa pato, wenzetu China wameendelea kutokana kutoipa nafasi mitandao kuihairbu China yao, wameipa nafasi kwa ajili ya kutangaza biashara na utalii, sasa sisi tumeipa nafasi kwa jili ya umbea”,.

Steve Nyerere ametoa kauli hizo zote kutokana na watu kuzusha taarifa kuwa mke wake amemkimbia, baada ya kugundua amezaa nje ya ndoa na muigizaji Welu Sengo.

Loading...
Chanzo: bongo5.com