Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria hawakamatiki Spotify, Bongo hakuna hata msanii mmoja

Selena Na Rema.jpeg Nigeria yafunika Spotify, Bongo hakuna hata msanii mmoja

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastaa wa muziki nchini Nigeria wanazidi kukimbiza kwenye mauzo kutokana na idadi ya wasikilizaji (streams) kwenye (digital platform) jukwaa maarufu la kidigitali la kutirisha maudhui ya muziki duniani, maarufu kama Spotify.

Katika orodha ya wasanii 30 waliosikilizwa zaidi kwenye mtandao huo wafuasi active milioni 600 kila mwezi, Tanzania haina msanii hata mmoja wakati Afrika Mashariki ikiwakilishwa na msanii mmoja tu, Sofiya Nzau kutoka Kenya mwenye streams zaidi ya milioni 3.4 kwa mwezi.

Rema kuroka Nigeria ndiye msanii anayeongoza akiwa na streams milioni 31.7, Tyla wa Afrika Kusini nafasi ya pili na Burna Boy nafasi ya tatu wakati Tems wote wa Nigeria akishika nafasi ya nne.

Africa's Most Spotify Monthly Listeners (Update)

1. Rema - Nigeria - 31.7 million

2. Tyla - Afrika Kusini - 28.1M

3. Burna Boy - Nigeria - 18.6M

4. Tems - Nigeria - 14.9M

5. Ayra Starr - Nigeria - 10.9M

6. Soolking - Algeria - 10.4M

7. Libianca - Cameroon - 9.9M

8. Wizkid - Nigeria - 9.59M

9. CKay - Nigeria - 9.58M

10. Davido - Nigeria - 8.7M

11. Omah Lay - Nigeria - 7.9M

12. Fireboy - Nigeria - 7.7M

13. Amaarae - Ghana - 6.9M

14. Seether - Afrika Kusini - 6.8M

15. Victony - Nigeria - 6.7M

16. Asake - Nigeria - 6.35M

17. Oxlade - Nigeria - 5.3M

18. Lojay - Nigeria - 5.18M

19. Tempoe - Nigeria - 5.17M

20. Kizz Daniel - Nigeria - 4.8M

21. Obongjayar - Nigeria - 4.6M

22. BNXN - Nigeria - 4.2M

23. Sherine - Misri - 4.1M

24. Sarz - Nigeria - 4.1M

25. Olamide - Nigeria - 3.9M

26. K'Naan - Somalia - 3.609M

27. Master KG - Afrika Kusini - 3.606M

28. Mr Eazi - Nigeria - 3.6M

29. Sofiya Nzau - Kenya - 3.4M

30. Young Jonn - Nigeria - 3.2M.

Spotify imekuwa chachu kubwa kwa wasanii wa Nigeria kufanya vizuri Kimataifa kwani ni mtandao Mtandao namba moja Duniani kwa Streams za muziki na maudhui ya sauti.

Pia, Spotify imekuwa ikiwapa nguvu wasanii wa Nigeria na baadhi ya wasaniii wa Afrika Kusini kwenye shoo zao za nje hasa kutokana na ngoma zao kukimbiza na kuwa maarufu kwenye mtandao huo.

Spotify inapatikana katika sehemu nyingi za Ulaya, na pia Afrika, Amerika, Asia na Oceania, na inapatikana katika masoko 184 kwa maana ya mataifa hivyo kupanua wigo wa wasanii kupenyeza kazi zao na kupiga mkwanja mrefu.

Watumiaji na waliojisajili, kwa sehemu kubwa wako nchini Marekani na Ulaya, wakichukua kwa pamoja karibu 53% ya watumiaji na 67% ya mapato ambayo wasanii wanalipwa.

Nini kifanyike ili wasanii wa Bongo waweze kupiga mkwanja kupitia digital platform hii kubwa Duniani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live