Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niffer adaiwa kuzama penzi la Patrick Kanumba

Kanumba Na Niffer Niffer adaiwa kuzama penzi la Patrick Kanumba

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo mfanyabishara na maarufu kwenye mitandao, Niffer anadaiwa kuwa yupo kwenye penzi zito na Patrick Kanumba aka Ochu au Othuman.

Licha ya Niffer mwenyewe kutotaka kuweka bayana hilo lakini mahojiano aliyoyafanya juzikati na Wasafi TV, yamedhihirisha kwamba huwenda wawili hao sio siri, kuna kitu!

"Ochu ana 25, mimi nina miaka 23. alipost Instagram, Ochu is my friend. Ni mtu ambaye ni mzuri anajua vitu vingi ananishauri vingi. Tulikutana 2020 KFC tukala piza basi," alisema Niffer huku akidai licha ya kujua umri wake na mambo mengine, wao ni marafiki tu.

Alipoulizwa Ochu huwa ananyoa saluni gani, Niffer alijisahau akataka kuitaja salani anayonyoa kisha akajishtukia katikati na kufumba mdomo kuashiria amevujisha siri ya kambi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live