Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niffer: Ninamiliki milioni 100, sidangi!

Niffer Jk Niffer: Ninamiliki milioni 100, sidangi!

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjasiriamali na mwanamitindo maarufu mitandaoni Niffer amefunguka kuwa yeye sio kama waadada wengine wa mjini wanaotegemea kutunzwa na wanaume, badaya yake anapambana katika biashara zake kujipatia kipato halali.

Niffer amefunguka hayo wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Lavidavi chini ya mtangazaji Diva kinachoruka kupitia Wasafi FM.

"Nimefanya biashara kwa muda mrefu na nilianza na mtaji mdogo, ila sasa hivi maisha yangu yote nina miliki mali na utajiri wa zaidi ya milion 100.

"Watu wengi hasa hapa Bongo wakiona Msichana mdogo ana pesa wanahisi anadanga... Mimi sidangi nafanya kazi sana, nalala masaa matatu tu.

"Safari yangu ya Dubai nilifikia hoteli ambayo kwa usiku moja ni shilingi milioni 2. Nilikaa siku 5 tu kisha nikaenda Afrika Kusini kwa ajili ya biashara. Siku 5 nikiwa Dubai kwa hoteli tu nilitumia milioni 10, nilitoa mwenyewe hakuna sponsor wala nini," amesema Niffer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live