Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niffer: Nina vigezo vyote vya kutoka na Kiba

NIFFER ALIKIBA Niffer: Nina vigezo vyote vya kutoka na Kiba

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo Niffer ameamua kufunguka kuhusu tetesi za kuwahi kuwa kwenye penzi na mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba wakati akihojiwa katika Kipindi cha Lavidavi cha Wasafi FM.

Akizungumzia hilo, Niffer anasema; "Sijawahi kuwa kwenye mahusiano na Ali, walituhusisha kwenye mahusiano sababu Ali ni handsome na mimi ni beautiful, ana taste yake ya wanawake na mimi nina taste yangu ya wanaume.

“Mimi ni miongoni mwa wanawake anaoweza kutoka nao, asingekuwa maarufu na kwenye ndoa ningetoka nae, nina vigezo vyote vya kutoka nae.

"Kinachonivutia kwa Ali, ni Muislamu, yuko charming, akiwa rafiki yako uta-enjoy urafiki wenu for life, Ali alikuwa mtu wa kwanza kunifariji nilivyoanza kuonewa mtandaoni baada yeye kuni-tag kwenye birthday post yake," amesema Niffer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live