Rapa Nicki Minaj amejikuta kwenye shutuma zisizo za kweli baada ya mtu mmoja kupiga simu polisi na kuripoti kuwa mtoto wa Nicki alikuwa akifanyiwa unyanyasaji nyumbani kwake L.A.
Inadaiwa kuwa kituo cha huduma kwa watoto walipokea simu kutoka kwa mtu asiyejulikana akidai kuna unyanyasaji wa mtoto nyumban kwa Nicki.
Maafisa wa polisi walifika nyumbani kwa Nicki kwenye mida ya saa 12 asubuhi kufuatilia jambo hilo, baada ya kufika walimkuta Nicki na mumewe Kenneth Petty na kuongea nao Kisha waligundua kulikuwa hamna unyanyasaji wowote nyumbani hapo.
Inadaiwa ilikuwa ni prank ( mchezo wa mzaha/masihara) uliofanywa na huyo mtu aliyepiga simu kuripoti tukio hilo lisilo la kweli.