Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nick Canon anatumia Milioni 500 kuwalipia Watoto kwenye Bustani

Nick Canon With Family Nick Canon anatumia Milioni 500 kuwalipia Watoto kwenye Bustani

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji na Mwanamuziki Nick Cannon, ambaye ana watoto 12, amesema anatumia karibu ($200,000) zaidi ya TSh. Milioni 500 kwa mwaka kwenye Disneyland, bustani maarufu ya kitalii iliyopo California, nchini Marekani.

Rapa huyo na mtangazaji wa Televisheni alikiambia kipindi cha redio cha The Breakfast Club kwamba yeye huenda Disneyland angalau mara moja kwa mwezi kuadhimisha matukio maalum kama vile siku za kuzaliwa za watoto wake na kwa tafrija za likizo.

Kiasi hicho kinakuja kutokana viingilio pamoja na gharama kubwa za hoteli katika eneo hilo maarufu duniani.

Kwenye mahojiano hayo, Cannon aliongea kwa malalamiko juu ya gharama hizo akieleza kwamba awali alikuwa akiingia bure kwani alikuwa mfanyakazi wa eneo hilo (2009-2013) na alikuwa na watoto wawili tu, Moroccan na Monroe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live