Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nick Cannon akatia Korodani zake bima ya Bilioni 26

Nick Cannon Balls Nick Cannon akatia Korodani zake bima ya Bilioni 26

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji na mtangazaji wa TV maarufu nchini Marekani, Nick Cannon, ameweka bima ya korodani zake kwa $10m (sawa na shilingi Bilioni 26 za kitanzania).

Cannon ameamua kufanya hivyo baada ya kutimiza idadi ya watoto 12 aliozaa na wanawake sita tofauti.

Gazeti la Daily Mail limeripoti kwamba muigizaji huyo aliishirikisha kampuni ya uuzaji wa bidhaa za kiume (Dr. Squatch), ambayo ilizifanyia tathmini korodani hizo kabla ya kuzikatia Bima.

Kwenye taarifa yake, Nick alisema: "Wanaochukia wanasema ni wakati wa mimi kuacha kuendelea kuzaa, lakini nimeamua kuongeza maradufu thamani ya korodani zangu na watoto wangu wa baadae.

“Pongezi kwa Dk. Squatch kwa kuzipa korodani zangu sifa inayostahili na kuniunganisha na ulinzi ninaohitaji ili kuendeleza mti wa familia”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live