Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni mwisho wa Asake na Lebo yake ya YBNL?

ASAKE Mwimbaji Asake

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji Asake, amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya hivi karibuni kufuta picha zote kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram na kufuta maandishi kwenye Bio yake, gumzo limekuja baada ya kufuta maneno yaliyokuwa yanaashiria kuwa ni mwanafamilia wa lebo ya “Yahoo Boy No Laptop” (YBNL) Inayomilikiwa na msanii Olamide na kuacha maswali kwa mashabiki kama ameacha kufanya kazi na lebo hiyo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram yenye wafuasi milioni Tano Mwimbaji @asakemusic ame post clip ya video ya wimbo unaojulikana “Stubborn” alioshirikishwa na msanii Victony, Asake alisainiwa na Olamide kupitia Lebo Ya “YBNL” mwezi Feb,2022 na kujipatia umaarufu wa ndani na nje ya bara la afrika kupitia kazi zake za muziki.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi inayosema kuwa Asake ametoka kwenye Lebo Ya YBNL

Chanzo: www.tanzaniaweb.live