Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni miaka minne sasa tangu kifo cha Pop Smoke

Murder Pop Smoke Ni miaka minne sasa tangu kifo cha Pop Smoke

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa marehemu Bashar Barakah Jackson maarufu kama Pop Smoke aliuawa akiwa na umri wa miaka 20 kwa kupigwa risasi na majambazi Februari 19, 2020 akiwa nyumbani kwake alipokuwa amekodi huko Hollywood Hills .

Majambazi hao walijua anwani alipokuwa akiishi kwa sababu siku moja mapema, Jackson alikuwa amechapisha picha kwenye mtandao wa kijamii ya begi la zawadi alilopokea na anwani yake ilikuwa kwenye lebo.

Wakati wa wizi ndipo rapa huyo Pop smoke aliuawa kwa kupigwa risasi na washambuliaji walifanikiwa kuiba saa ya Jackson ya Rolex na kuiuza kwa $2000 zaidi ya Tsh Milioni 5.

Hivyo jana Februari 19 ilikuwa ni kumbukizi (Anniversary) ya kifo chake ikiwa ni miaka 4 imepita tangu atutoke.

Tuambie wimbo gani wa Pop Smoke unaukubali zaidi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live