Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni kweli Zuchu ametia aibu mbele ya Spika?

Diamond Zuchu Ma Ni kweli Zuchu ametia aibu mbele ya Spika?

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni aibu iliyoje? Ndivyo baadhi ya wahudhuriaji walivyosikika wakisema kufuatia vitendo vya aibu walivyovionesha msanii Zuchu na bosi wake, Diamond Platnumz mbele ya viongozi wakubwa nchini wakiongozwa na Spika, Mawaziri na Wabunge.

Tukio hilo lilijiri mapema wiki hii katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, wakati wa uzinduzi wa Albam ya Love Sounds Different ya msanii Barnaba Boy Classic ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson.

Gazeti la IJUMAA lilikuwa sehemu ya wahudhuriaji wa shughuli hiyo ambapo liliwashuhudia baadhi ya watu wakijionea aibu kutokana na jinsi Zuchu alivyojiachia jukwaani na Diamond huku wakifanyiana vitendo vya kimahaba hadharani.

Zuchu alishuhudiwa akisasambua kigauni chake cha chukuchuku cha rangi ya kijani au mgomba akiwa jukwaani na kumuachia Diamond kumkamatia hadi maeneo hatarishi ya mwili wake.

Baadhi ya watu wanasema kuwa, kuna wakati mikono ya Diamond ilivuka mipaka na kusababisha baadhi ya watu kutazama pembeni wasione kilichokuwa kinaendelea. Wawili hao walifanya hivyo wakati wakipafomu nyimbo zao mbalimbali kama Fire, Litawachoma na nyinginezo.

Wakati wote wakicheza, Zuchu alikuwa anainama na kuacha sehemu kubwa ya mwili wake kuwa wazi kiasi cha watu wenye heshima zao kuona aibu kidizaini f’lani.

Hivi sasa imekuwa ni nadra mno kumuona Diamond kwenye tukio kubwa nchini na hata nje ya nchi bila Zuchu na mahaba yao hivi sasa hawana aibu hata tone.

Baadhi ya watu waliozungumza na Gazeti la IJUMAA walisema kuwa, alichokifanya Zuchu ilikuwa ni kukomesha kabisa ili kama kuna mwanamke anayetaka kujipendekeza kwa Diamond, basi ajue yeye yumo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live