Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni Diamond na mrembo mpya kwenye headlines za mapenzi

Diamond Ris Diamond na Ms Ris Eddy.

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

STAA wa mziki wa bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz inadaiwa kwamba yupo visiwani Zanzibar na mwanadada kutokea nchini Rwanda anayefahamika kwa jina la Ms Ris Eddy.

Taarifa za Diamond kutoka kimapenzi na mwanadada huyo msomi kutokea Rwanda zimeanza kusambaa kupitia mitandao ya kijamii hii jana, Septemba 27, 2021.

Lakini pia, taarifa hizo zilithibitishwa zaidi, baada ya mrembo huyo kuweka video fupi kupitia Insta story yake akiwa katika hotel inayosadikika kuwa ipo Zanzibar huku pia Diamond Platnumz akisambaza video inayoonyesha mazingira yanayofanana kama ya mwanadada huyo, ndipo gumzo na mzozo mkubwa ukawa umetanda katika mitandao ya kijamii.

Ifahamike kuwa mrembo Ris Eddy ni msomi aliyewahi kusoma katika chuo cha UDSM Jijini Dar es Salaam na pia nchini Uingereza, katika masomo ya Uongozi wa Biashara.

Dimaond Platnumz kwa kipindi kirefu tokea alivyotengana na mama mtoto wake Tamasha Donna kutoka nchini Kenya, alikuwa bado hajatutambulisha mwanamke wake mwingine, lakini Ris Eddy ndiye anatajwa kurithi mikoba ya Tanasha kwa Mondi.

Katika kulithibitisha hilo pia, mtu wa karibu na familia ya Diamond, Juma Lokole amekuwa akituma picha na video mbalimbali za mrembo Ris Eddy ambazo zinaonyesha mwanadada huyo upo katika gari jipya ambalo linasemekana kwamba amenunuliwa na Diamond Platnumz pia.

Bado taarifa hizi haijathibishwa na Diamond Platnumz mwenyewe japo lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja. Acha tusubiri mapenzi siku zote ni kikohozi hauwezi kuyaficha hata siku moja na itafahamika tu siku moja juu ya tetesi za penzi hili. Alizanza Bongo (kwa Wema), akaenda Uganda (kwa Zari), akarudi Bongo (kwa Mobetto), akaenda Kenya (kwa Tanasha) na sasa ametua Rwanda (kwa Ris).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live