Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni Bob Junior kwenye spika za radio yako tena

A62141cb9ae78e77573e8f8ae65fd762 Mwimbaji na Mtayarishaji Muziki, Bob Junior

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BAADA ya kimya cha muda mrefu, nyota wa muziki wa kizazi kipya Raheem Rummy ‘Bob Junior’ ameachia wimbo mpya wa Itetemeshe alioumba kwa ushirikiano na msanii kutoka lebo ya Wasafi Abdul Idd ‘Lavala- va’.

Bob Junior ambaye pia, ni mtayarishaji wa muziki kutoka rekodi ya Sharobaro, alishindwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya muziki wa kisasa hapo nyuma na kupotea kidogo.

Licha ya kwamba alitoa baadhi ya nyimbo miaka ya hivi karibuni, bado hakuvuma sana kama ilivyokuwa miaka ya 2011 hadi 2012, ambapo alikuwa akifanya vizuri.

Baada tu ya kutoa wimbo huo aliomshirikisha Lavalava, jana aliandika ujumbe kupitia mtandao wake wa Instagram kuwa kazi hiyo ni moja ya kitu bora katika maisha yake.

“Wimbo huu ni moja ya kitu bora katika maisha yangu nikifanya muziki mzuri hususani nikipata nafasi yakufanya kazi na mtu mwenye kipaji kama huyu mdogo wangu Lavalava,”alisema.

Alimshukuru Lavalava kwa kumpa heshima ya kutoa wimbo huo akiamini ni moja ya kazi bora kwake na hivyo, kuwaomba mashabiki kumuunga mkono. Msanii huyo kabla ya kuachia wimbo huo alihusika kuandaa wimbo wa Revokatus Kipando ‘Baba Levo’ wa Amapiano, ambao ulifanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali na sasa amerudi kwa kutoa wimbo wake

Chanzo: www.habarileo.co.tz