Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nguza aelezea alivyopokea kifo cha Magufuli

A80ba8013c10a801cd89717ad06b83f8 Nguza aelezea alivyopokea kifo cha Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI nguii nchini, Nguza Viking au Babu Seya amesema kuwa alikuwa haamini kama kweli aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli amefariki dunia.

Babu Seya alihukumiwa kifungo cha maisha jela kabla ya kupata msamaha wa Rais Magufuli baada ya kutumikia kifungo hicho kwa miaka kadhaa.

Alisema kuwa tangu Magufuli afariki amekosa usingizi kwa jinsi akikumbuka aliyomfanyia.

Alisema kuwa alipata mshtuko mkubwa aliposikia kuwa Magufuli amefariki dunia, ambapo aliwataka Watanzania kuwa wavumilivu, kwani Mungu atatusaidia.

Alisema kuwa taarifa za msiba alizipata kupitia kwa mtoto wake Papii akimtaka baba yake kuangalia mtandao, kwani Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu alikuwa akitangaza kifo cha Dk Magufuli katika TV.

“Mimi sijalala niliposikia kifo cha Magufuli, Papii alinipigia simu akitaka niangalie mitandao, kwani Mama Samia alikuwa akitangaza kifi taarifa hiyo, nilishtuka sana na hata mimi ningeweza kupoteza maisha, “alisema.

Aliongeza kuwa Rais hajafa kwani ataendelea kuwepo kiroho katika miaka yote kutokana na matendo yake mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

Alisema kuwa Rais Magufuli hajafa…yupo kwani vitendo vyake vitaendelea kuwepo siku zote.

Chanzo: www.habarileo.co.tz