Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nguo za Kanye West zaibiwa

Kanye West@2000x1500 1 Nguo za Kanye West zaibiwa

Sat, 16 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu’ ya wafanyakazi katika kampuni ya mwanamuziki Kanye West, Ye’s imeripoti kuwa zaidi ya nguo zenye thamani ya dola 1 milioni zimeibiwa kwenye ghala la nguo la kampuni hiyo lililoko Las Angeles nchini Marekani.

Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa wafanyakazi kampuni ya Ye’s Milo Yiannopoulos, ambapo aliiambia Tmz kuwa wafanyakazi waligundua kiasi kikubwa cha nguo za ‘Yeezy GAP’ kwenye ghala la Ye’s zilipotea siku chache zilizopita ambapo wamedai kuwa takribani nguo 60,000 zimeibia, zenye thamani ya dola 1.2 milioni.

Aidha Yiannopoulos alieleza kuwa ‘timu’ yake ya wafanyakazi haikujua nguo hizo zilikwenda wapo, lakini waligundua kuwa zimeibiwa baada ya kuona akaunti ya shabiki wa Kanye akiuza nguo hizo za Yeezy GAP kwa dola 20.

Hata hivyo Yiannopoulos amedai kuwa tayari wamemtambua mmoja wa wezi waliuhusika katika wizi huo hivyo atashirikiana na polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live