Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nguo ya ndani yamponza Jux, mashabiki wamchana vibaya!

JUX Boksa Nguo ya ndani yamponza Jux, mashabiki wamchana vibaya!

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wabongo wewe wawekee picha tu, maelezo wanayo wenyewe! Ndicho kilichomkuta staa wa Bongo Fleva Jux baada ya kuposti picha yake katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amevaa nguo ya ndani pekee (boksa).

Kwenye picha hiyo, Jux alisindikiza na ujumbe wa Kingereza akimaanisha kwamba boksa yake hiyo safi na smati na inawavutia wanawake wengi.

“A Clean and a Smart boxer is a major turn on to a lot of women.”

Sasa baada ya ujumbe huo, Wabongo wakaanza kumvaa sasa kwa kumuambia inakuwaje atupie picha inayomuonesha live ‘mzigo’ wake.

Wengine walienda mbali zaidi kwa kumuambie afute kwani siyo maadili ya Kitanzania huku wengine wakimuambia mambo ya kuiga sio mazuri. Hata hivyo Jux hajaifuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live