Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nguo ya ndani ya Zuchu yazua mjadala

Zuchu Na Diamond Nguo Ndani Nguo ya ndani ya Zuchu yazua mjadala

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hapana shaka sasa hivi Zuhura Othuman ni miuongoni mwa warembo ambao wanafanya vizuri kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, kila siku anafanya ngoma kali na kuzungumzwa zaidi.

Miongoni mwa matukio ambayo yanamfanya aibue mjadala kwa sasa ni kufuatia kitendo chake cha kuvaa suruali huku ikiacha sehemu kubwa ya nguo yake ya ndani (bikini) ikiwa wazi.

Picha hiyo inamuonesha Zuchu akiwa ameshikwa kiuno na Diamond Platnumz huku bibie akionekana kutojali sana maana sasa hivi kashamzoea sana bosi wake huyo ambaye anahusishwa kuwa na mahusiano nayo yasiyo ya kindugu.

Mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii inahoji kulikoni mtoto wa Kiislamu mwenye mama yake ambaye anajiheshimu (Khadija Kopa) inakuwaje anaonesha nguo hiyo ya staha kwa watu wote?

“Huyu ndo bosi huyu mtoto wakiislam unaacha chu** nje hivyo duu Hadija Kopa anaangalia tu,” alichangia mtu anayejiita tatuabdalla4 katika mtandao wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live